Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gavana wa benki kuu Nigeria afikishwa mahakamani

Gavana Wa Benki Kuu Nigeria Gavana wa benki kuu Nigeria afikishwa mahakamani

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: Voa

Gavana wa benki kuu ya Nigeria Godwin Emefiele aliyekuwa amesimamishwa kazi, alifikishwa mahakamani Jumanne ambapo amekana mashitaka ya kumiliki bunduki na risasi kinyume cha sheria, ikiwa ni mara ya kwanza, baada ya zaidi ya mwezi mmoja kuonekana hadharani.

Emefiele aliwekwa kizuizini na idara ya usalama wa taifa tarehe 10 Juni, siku moja baada ya rais mpya Bola Tinubu kumsimamisha kazi.

Mwezi huu, Jaji aliamuru idara hiyo kuwasilisha mashtaka kuhusiana na tuhuma hizo au kumwachilia gavana huyo. Emefiele, akiwa amevaa kaftan nyeupe, akionekena dhaifu, alikana mashtaka mawili ya kumiliki silaha na risasi kinyume cha sheria, mwandishi wa shirika la habari la Reuters alisema. Amepinga kuzuiliwa kwake na kuwasilisha maombi ya dhamana.

Mahakama Jumanne ilimpa Emefiele dhamana kwa masharti ya kulipa naira milioni 20 na kusema anapaswa kuwekwa rumande hadi masharti ya dhamana yatakapotimizwa au hadi tarehe 14 Novemba kesi yake itakaposikilizwa.

Mawakili wa serikali waliiomba mahakama mwezi Juni kuidhinisha kuzuiliwa kwa Emefiele kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na "uvunjaji wa uaminifu wa jinai," mashtaka ambayo adhabu yake ni kifungo kirefu endapo yatathibitishwa.

Waliweza kupata agizo la mahakama la kumshikilia Emefiele wakati wakisubiri uchunguzi zaidi. Emefiele alijulikana kwa kutumia sera zisizo za kawaida ili kuweka sarafu ya naira ya nchi kuwa imara na kutoa mikopo ya moja kwa moja kwa biashara ili kujaribu kukuza ukuaji.

Rais Tinubu, ambaye anaanza mageuzi ya ujasiri mkubwa katika nchi hiyo yenye uchumi mkubwa zaidi barani katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja, Tinubu alikosoa sera za benki kuu ambayo ilikuwa chini ya Emefiele wakati alipoapishwa mwezi Mei, akisema walihitaji "kusafisha nyumba vizuri," bila kutoa maelezo.

Chanzo: Voa