Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gavana wa Sudan awataka raia kuulinda mji wa El Fasher uliyozingirwa

Gavana Wa Sudan Awataka Raia Kuulinda Mji Wa El Fasher Uliyozingirwa Gavana wa Sudan awataka raia kuulinda mji wa El Fasher uliyozingirwa

Fri, 17 May 2024 Chanzo: Bbc

Gavana wa jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan, Minni Minnawi, amewataka raia kuchukua silaha ili kujilinda paona mji mkuu wa eneo hilo, El-Fasher, kutoka kwa Jeshi la Rapid Support Forces (RSF), ambalo limeuzingira mji huo kwa wiki kadhaa.

Zaidi ya watu 60 wamefariki na mamia kujeruhiwa tangu mapigano ya hivi punde yalipoanza tarehe 10 Mei, kulingana na shirika la misaada la kimatibabu la Madaktari Wasio na Mipaka.

"Tunatangaza tahadhari ya jumla ya kutetea maisha na mali ya raia wasio na hatia huko El Fasher," Bw Minnawi alisema katika chapisho kwenye mtandao wa X siku ya Alhamisi.

Alikuwa akijibu wito kama huo wa RSF, ambayo alisema "imezindua kampeni mpya ya kuhamasisha [wapiganaji] kutoka mikoa yote" kuvamia jiji hilo. RSF, hata hivyo, ilikataa madai hayo na badala yake ikamshutumu gavana huyo kwa "kuchochea mifarakano katika Darfur".

Vikosi vya kijeshi na jeshi la Sudan, likisaidiwa na makundi yenye silaha ya Darfur, wameendelea kulaumiwa kutokana na kuongezeka kwa mapigano ya hapa na pale huko El Fasher.

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Clementine Nkweta-Salami, ameonya kwamba kuendelea kwa ghasia kunatishia maisha ya watu zaidi ya raia 800,000.

Vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan vilianza mwezi Aprili mwaka jana na juhudi za kimataifa za kusuluhisha mapigano kati ya vikosi hasimu zimetibuka mara kwa mara.

Chanzo: Bbc