Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gavana wa Sudan atoa wito kwa Darfur kuchukua silaha

Gavana Wa Sudan Atoa Wito Kwa Darfur Kuchukua Silaha Gavana wa Sudan atoa wito kwa Darfur kuchukua silaha

Fri, 21 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Gavana wa Darfur na kiongozi wa zamani wa waasi Minni Arko Minnawi amerudia wito wake kwa raia katika eneo hilo kuchukua silaha ili kujilinda, akisema "hali ya sasa inalazimu hilo", Chombo cha habari Al Arabiya kimeripoti.

Alisema utawala huu ulikuwa unaongoza juhudi za kusitisha mapigano kati ya Rapid Support Forces (RSF) na jeshi, haswa huko Darfur.

Mzozo huo sasa uko katika mwezi wake wa nne.

Bw Minnawi ametoa matamshi sawa na hayo siku za nyuma, na kuzua hofu kwamba Darfur, ambayo imegawanywa katika majimbo matano, inaweza kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe huku kukiwa na ongezeko la mivutano ya kikabila.

Kwingineko nchini humo, mapigano makali yaliripotiwa kati ya jeshi na RSF huko Khartoum, Omdurman na Bahri, miji mitatu inayounda mji mkuu wa Sudan.

Walioshuhudia mjini Khartoum walisema jeshi lilifanya mashambulizi "makali zaidi ya anga" kuwahi kushuhudiwa dhidi ya vikosi vya RSF katika maeneo kadhaa. Jeshi lilisema kuwa liliwaua wapiganaji 18 wa RSF katika mapigano huko Omdurman na Khartoum.

Mapigano mapya pia yaliripotiwa huko Nyala, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kusini, baada ya mapigano kutulia.

Mapigano hayo yameendelea licha ya kufanyika kwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya jeshi na wawakilishi wa RSF katika mji wa Jeddah wa Saudia.

Chanzo: Bbc