Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gavana wa Kenya amsaidia kijana wa miaka 14 aliyesafirishwa kutoka Burundi

Gavana Wa Kenya Amsaidia Kijana Wa Miaka 14 Aliyesafirishwa Kutoka Burundi Gavana wa Kenya amsaidia kijana wa miaka 14 aliyesafirishwa kutoka Burundi

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Gavana wa mji mkuu wa Kenya, Nairobi, amemsaidia mvulana wa miaka 14 wa Burundi ambaye alihangaishwa na maafisa wa kaunti kwa kosa la kuchuuza njugu karanga mitaani.

Video za mvulana huyo akilia baada ya maafisa wa kaunti kudaiwa kumwaga njugu zake mtaani zilisambaa siku ya Jumanne, na kuibua hisia za huruma kwa mvulana huyo na ghadhabu dhidi ya maafisa wa kaunti.

Ilisababisha hatua kutoka kwa Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja, ambaye alifichua Jumatano kwamba mvulana huyo alikuwa ni raia wa Burundi aliyesafirishwa kwenda kufanya kazi kama mchuuzi nchini Kenya.

Aliongeza kuwa amekuwa na mazungumzo na balozi wa Burundi ili kijana huyo aanze shule.

Hata hivyo, alikanusha madai ya unyanyasaji, akisema kuwa maafisa wa kaunti walikuwa wakimzuia mvulana huyo kurandaranda nje ya saa zilizopangwa.

"Kwa bahati mbaya, wakati (yeye) alikamatwa na afisa wa utekelezaji kuizilia bidhaa zake, mtoto huyo mdogo alijitahidi kuishikilia ndoo, akamwaga chini njugu ," aliongeza.

Bw Sakaja alisema atashirikiana na wizara ya mashauri ya nchi za kigeni kushughulikia ongezeko la ulanguzi wa watoto na uhamiaji haramu.

Mamlaka hapo awali zilisema kuwa wageni, ikiwa ni pamoja na watoto na watu wenye ulemavu, wanasafirishwa kwenda kufanya kazi nchini Kenya, mara nyingi kama ombaomba au wachuuzi.

Chanzo: Bbc