Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gavana Joho kuwania urais 2027, aashiria Raila atatengeneza njia 2022

0fgjhs189rjkpqra28 Gavana Joho kuwania urais 2027, aashiria Raila atatengeneza njia 2022

Tue, 26 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Raila Odinga ana matumaini ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya mwaka wa 2022 licha ya kushindwa katika chaguzi nne zilizopitaGavana Hassan Joho ameashiria kwamba wakati wa Raila kuwa Rais umewadia na atatawala kwa muhula mmoja pekee.

Kulingana na Joho, Raila akiwa Rais 2022, atasafisha na kutengeneza njia yake kuwa rais mwaka wa 2027Gavana wa Mombasa Hassan Joho amedokeza kwamba Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga atakuwa Rais mwaka wa 2022 ila kwa muhula mmoja pekee.

Akizungumza na wanahabari wa runinga ya K24 Oktoba 26, Joho aliwarahi wananchi haswa wakazi wa eneo la Pwani kumuunga mkono Raila katika uchaguzi mkuu wa 2022 ili iwe rahisi kwake yeye kuwania urais mwaka wa 2027.

Kulingana na Joho, Raila akiwa Rais 2022, atasafisha na kutengeneza njia yake kuwa rais mwaka wa 2027.

" Nataka Baba ashinde uchaguzi wa 2022 ili mwaka wa 2017 aniwachie nafasi ya kuwania urais nami pia," Joho alisema akiashiri kwamba Raila ataongoza kwa muhula mmoja pekee.

Joho ambaye alimuachia Raila nafasi ya kuwania kiti cha urais aliwaonya pia wakazi wa eneo la Pwani dhidi ya kuabiri wilbaro akisema hatua hiyo huenda ikaathiri viongozi wao kupata vyeo vya juu serikalini.

"Mwanasiasa mwingine ambaye sio wa chama cha ODM akishinda uchaguzi, hamtawahi kukiona tena kiti cha urais,"Aliongezea Joho akiashiria Naibu Rais William Ruto.

Raila ambaye amekuwa akijaribu bahati ya kuwa Rais, atakuwa debeni kwa mara ya tano kumenyana na naibu Rais William Ruto na viongozi wengine ambao wametangaza azma ya kuwania kiti hicho.

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kustaafu mwaka wa 2022 baada ya kuwa madarakani kwa mihula miwili, hata hivyo hajatangaza mrithi wake ila amekuwa akionyesha dalili za kumuunga mkono Raila.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke