Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gavana Joho asafiri kwa ndege ya kifahari baada ya kushambuliana na Safarilink

094acd04057f2d9a Gavana Joho asafiri kwa ndege ya kifahari baada ya kushambuliana na Safarilink

Sat, 22 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Gavana Joho alichapisha ujumbe mitandaoni akilalamika baada ya kuachwa na ndege Ijumaa, Mei 21

- Joho alisuta vikali usimamizi wa Safarilink juu ya kile alichokitaja kuwa utepetevu kazini licha ya kuwepo kwa ushindani katika safari za anga

- Muda mfupi baadaye alipakia video kwenye Instagram akionesha akisafiri katika ndege ya kifahari

Gavana wa Mombasa Hassan Ali Joho amesonga mbele na maisha baada ya kulalamika vikali baada ya ndege ya shirika la Safarilink kumwacha katika uwanja wa Vipingo.

Mnamo Ijumaa,Mei 21, mwanasiasa huyo bwenyenye kutoka Pwani alichapisha ujumbe mitandaoni wa kulisuta vikali shirika hilo baada ya kuachwa katika uwanja wa ndege.

Katika ulimwengu wa sasa ambapo kunao ushindani mkali katika safari za ndege, hamna nafasi ya mtu kuonesha utepetevu kazini jinsi usimamizi wa Safarilink ulivyofanya," alilalamika.

Hata hivyo usimamizi wa ndege hiyo ulimjibu mteja wake na kumkumbusha kwamba alichelewa na hivyo basi haingekuwa vyema kuwachelewesha wateja wengine waliokuwa tayari wamefika kwa wakati ufaao.

"Tunafahamu ulifika kwenye Uwanja wa Ndege wa Vipingo saa 16:04 ambapo tayari muda wa kuondoka ulikuwa umepita. Kama shirika la ndege tunaenda na wakati. Pia tunahitaji kuwaheshimu wateja wengine ambao tayari walikuwa wamepnada ndege tayari kuondoka," usimamizi wa Safarilink ulisema.

Shirika hilo lilipendekeza kuorodhesha tikiti ya gavana huyo hadi tarehe nyingine bila kumuadhibu kwa njia yoyote ile lakini jibu hilo lilionekana kumuudhi hata zaidi mwanasaiasa huyo.

Hata hivyo baada ya hali kutulia, gavana huyo aliamua kusafiri akitumia ndege ya kibinafsi ya kifahari ambapo alipakia picha kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Gavana huyo alionekana akisafiri kwenye ndege hiyo ya kifahari, labda ya kikosi chake kizima.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke