Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gari lenye mwili wa marehemu lateketea kwa moto

Gariiiia75c.jpeg Gari lenye mwili wa marehemu lateketea kwa moto

Sat, 16 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msafara wa mazishi ulilazimika kusimama ghafla gari lililokuwa limebeba mwili wa marehemu kuwaka moto na kuteketea kabisa.

Gari hilo jeusi aina ya Mercedes Benz lililokuwa likielekea kwenye mazishi limeibua simanzi upya baada ya kuteketea licha ya juhudi za kuuzima moto huo, gari hilo lililokuwa la kifahari liliteketea ma kubaki jivu.

The Mirror inaripoti kwamba tukio hilo la kushangaza lilitokea huku waombolezaji na wahudumu wa dharura wakihangaika kuokoa hali.

Maelezo yanaonyesha kuwa Mercedes hiyo nyeusi ilikuwa ikisafiri Church Stretton, Shropshire, iliposhika moto mwendo wa saa saba adhuhuri.

Picha za kustaajabisha zilinasa gari la kubebea maiti likiwaka moto muda mfupi baada ya jeneza kuvutwa kutoka kwenye hatari na waombolezaji na wazima moto waliokuwa wameshuka.

Moto huo mkubwa uliacha gari lililokuwa la kifahari likiwa limeungua, lakini hakukuwa na majeraha yaliyoripotiwa, na jeneza halikuteketea katika kisa hicho.

Juhudi za haraka kutoka kwa wazima moto na familia ilichukua jukumu muhimu katika kudhibiti moto huo.

Msemaji kutoka kanisani alieleza kwamba mawazo na sala zake zilikuwa pamoja na familia hiyo.

Alipongeza kuwa juhudi za haraka ambayo yaliokoa familia kutoka kwa huzuni zaidi siku ambayo tayari ilikuwa na huzuni vya kutosha.

"Wafanyikazi na umma walifanikiwa kulitoa jeneza kwenye gari kabla ya kuteketea, ilikuwa ni juhudi ya kupongezwa kwa kila mtu aliyekuwa hapo," alisifu.

Matukio yasiyotarajiwa bila shaka yameongeza safu ya huzuni kwa tukio ambalo tayari la huzuni kwa familia inayoomboleza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live