Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gari la misaada lashambuliwa Sudan

Wanajeshi Wa RSF Sudan Watangaza Kusitisha Mapigano Kwa Ajili Ya Eid Gari la misaada lashambuliwa Sudan

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Msalaba Mwekundu limeripoti kuwa watu wawili wameuawa na wengine saba kujeruhiwa katika shambulio linalotajwa kama la makusudi dhidi ya msafara wa misaada ya kiutu katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo inasema jeshi na wanamgambo wa RSF waliwahahikishia usalama wafanyakazi wake wanaposafirisha mamia ya raia kuelekea maeneo salama lakini walishambuliwa.

Shambulizi hili limetokea baada ya viongozi wa kikanda kusema viongozi wa jeshi la Sudan na kikosi maalum cha wanamgambo cha RSF wamekubaliana kufanya mazungumzo ya amani na kusitisha vita ambavyo vimesababisha mauaji ya maelfu na kuwaacha watu milioni sita bila ya makazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live