Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gambia inafanya Uchaguzi Mkuu wa Kihistoria leo

Gambia Decides Gambia inafanya Uchaguzi Mkuu wa Kihistoria leo

Sat, 4 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya raia 960,000 wa Gambia wanapiga kura kumchagua rais wao mpya leo hii, Desemba ikiwa ni uchaguzi wa kwanza wa urais tangu Yahya Jammeh kushindwa 2016, baada ya miongo miwili ya utawala wa kimabavu.

Wagombea sita wanashiriki kwenye kinyang'anyiro hicho, akiwemo rais anayemaliza muda wake Adama Barrow na makamu wake wa zamani Ousainou Darboe, mpinzani wa kihistoria.

Uchaguzi huu unachukuliwa kuwa "jaribio" kwa demokrasia hii changa ambao unafanyika chini ya uangalizi wa waangalizi wa kitaifa na kimataifa.

Rais wa sasa Adama Barrow aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2016, ana matumaini ya kushinda muhula wa pili

Wagombea sita wanagombea kiti cha urais. Wachambuzi wanasema ushindani mkali ni kati ya wagombea wawili ambao ni Rais Adama Barrow wa chama cha NPP na aliyekuwa Naibu wake Ousainou Darboe anayegombea kwa tiketi ya chama cha United Democratic Party (UDP).

Gambia ni nchi changa kidemokrasia inakabiliwa na changamoto chungu nzima, kuanzia ukosefu wa ajira hasa miongoni mwa vijana, masuala ya afya, elimu, miundombinu, na uchumi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live