Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gambia:Kesi dhidi ya Ousman Sonko kuendelea nchini Uswisi

Sonko Gambia Gambia.png Gambia:Kesi dhidi ya Ousman Sonko kuendelea nchini Uswisi

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama nchini Uswisi katika uamuzi wake imeruhusu kuendelea kwa kesi dhidi ya waziri wa zamani nchini Gambia Ousman Sonko, anayehusishwa na madai ya mauaji, kuwatesa watu pamoja na kuwabaka wanawake.

Sonko kwa upande wake amekana madai hayo yanayodaiwa kutekelezwa wakati wa utawala wa rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh.

Mahakama hiyo hapo jana Jumanne, ilitupilia mbali ombi la mawakili wa upande wa utetezi kuwa haikuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Sonko alienda uhamishoni nchini Uswisi mwaka wa 2016 ambapo ameshtakiwa chini ya sheria inayoruhusu mtu kushtakiwa hata kama madai anayokabiliwa nayo yalifanyika kwengine.

Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa kwa kipindi cha mwezi mmoja kabla ya uamuzi kufanyika mwezi Machi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live