Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gachagua kama wewe ni Maumau lete ushahidi – Odinga

Odinga Hy.png Gachagua kama wewe ni Maumau lete ushahidi – Odinga

Thu, 8 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa Azimio la Umoja One – Kenya, na Mwenyekiti wa Chama cha ODM, Raila Odinga amemtaka Naibu Rais, Rigathi Gachagua kuthibitisha matamshi yake ya hadharani kuwa yeye ni mtoto wa MauMau.

Hatua ya Odinga imekuja bada ya Gachagua kusisitiza kuwa yeye ni mwana wa MauMau, kutoka vuguvugu la Mlima Kenya, lililosaidia Kenya kupata uhuru kutoka kwa serikali ya mkoloni.

Amesema, “ikiwa kweli wewe ni mtoto wa MauMau kama unavyodai, jitokeze uthibitishie Wakenya, na kiongozi wa wengi bungeni, Kimani Ichungwa naye atoe thibitisho kama ni mwana wa MauMau.”

Maumau kutoka Mlima Kenya, lilikuwa ni ‘jeshi la askari’ kutoka jamii ya eneo la Kati lililojificha msituni kukabiliana na askari wa mabeberu wa Muingereza na kusaidia Kenya kuwa huru mwaka 1963.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live