Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gachagua: Hata upige kelele kodi utalipa tu!

Naibu Ras Kenya Gachagua: Hata upige kelele kodi utalipa tu!

Fri, 3 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua amesema serikali haitarudi nyuma katika azimio la kuhakikisha wale wasiolipa kodi wanafanya hivyo kwa maendeleo ya taifa hilo.

Gachagua, ameeleza hayo leo Februari 2, 2023 ambapo amewtaka wananchi nchini humo kuhakikisha kila mmoja wao analipa kodi kwa wakati.

“Tunataka kumueleza Seneti kurudi kwa Rais na Watendaji katika kuhakikisha kwamba kila mtu lazima alipe ushuru, haijalishi wewe ni nani. Tunakwenda kuijenga nchi hii kwa rasilimali zetu kwa sababu tumeacha kukopa.” Amesema Gachagua.

Ameongeza kuwa hakuna mwananchi anayeweza kukimbia jukumu hilo, hata hivyo hakuna mwananchi atakayekwenda kufanya hivyo hata kama atapiga kelele kwa kiasi gani atalipa kodi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live