Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gabon: 21 washtakiwa kuzama kwa feri iliyoua makumi

D0D683B8 F08E 48D6 8D06 25F504E4044F.jpeg Gabon: 21 washtakiwa kuzama kwa feri iliyoua makumi

Sun, 9 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu 21 wameshtakiwa kwa kuuwa bila kukusudia katika uchunguzi wa ajali ya kuzama feri ndogo iliyouwa watu 30 na kusabababisha wengine 7 wakiwa hawajulikani walipo hadi sasa. Ajali hiyo ya feri ilitokea mwezi uliopita huko Gabon. Haya yameelezwa na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Gabon.

Tarehe 9 Machi mwaka huu feri kwa jina la "The Esther Miracke ambayo hufanya safari zake baina ya mji mkuu wa Gabon Libreville kuelekea mji wa Port-Gentil ilipinduka na kuzama majira ya usiku; ambapo abiria 124 waliokuwemo kwenye feri hiyo kati ya 161 waliweza kuokolewa.

Serikali ya nchi hiyo ndogo ya Afrika ya Kati ilifanya haraka kubainisha makosa makubwa yanayoweza kutokea kuhusu vibali vya huduma za safari za majini vilivyotolewa kwa meli hii ya abiria na mizigo inayomilikiwa na kampuni binafsi ya Royal Cost Marine (RCM).

Feri hiyo Ilizama kilomita kumi tu kutoka eneo la pwani. Aidha abiria walionusurika na ajali hiyo ya feri na familia za watu waliopoteza maisha wamekosoa kucheleweshwa zoezi la uokoaji mara baada ya kutokea kupinduka na kuzama feri hiyo tajwa.

Taarifa ya Wizara ya Usafirishaji na Uchukuzi ya Gabon imeeleza kuwa makumi ya watu walihojiwa katika seli ya polisi kama sehemu ya uchunguzi wakiwemo maafisa kutoka kampuni miliki ya feri ya The Esther Miracle.

Andre Patrick Roponat Mwendesha Mashtaka wa Gabon ameeleza kuwa: Kati ya "watu 48 waliofikishwa mbele ya Mwendesha Mashtaka tarehe 6 na 7 Aprili mwezi huu; 21 wameshtakiwa na Jaji anayechunguza kesi ya makosa ya kuua na kujeruhi bila kukusudia, kushindwa kutoa msaada, kughushi na kuhatarisha maisha ya wengine".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live