Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Funga Nchi Tena: Otiende Omollo Amwambia Rais Uhuru Kutokana na Covid-19 Kuenea

37fa073ffbc3b70c Funga Nchi Tena: Otiende Omollo Amwambia Rais Uhuru Kutokana na Covid-19 Kuenea

Thu, 25 Mar 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Otiende anataka baadhi ya kaunti zifungwe kama njia ya kukabiliana na kuongezeka kwa maambukizi ya Covid-19

- Alisema kuna haja ya hatua kali kuchukuliwa ili kukabiliana na wimbi la tatu la Covid-19

- Wizara ya Afya imetangaza kuwa ugonjwa unasambaa kwa haraka zaidi tangu wimbi la tatu kulipuka

Mbunge wa Rarieda Otiende Omollo amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kuweka sheria ya kutoingia au kutoka katika maeneo ambapo Covid-19 inapepea.

Akiongea na runinga ya Citizen Alhamisi Machi 25, Otiende alisema Rais anafaa kurudisha hatua kali zilizokuwa zimetolewa na serikali kukabili Covid-19.

"Ukiangalia baadhi ya maeneo kama vile Kiambu na Machakos maambukizi yako juu zaidi na ni lazima kafyu ya kutoingia au kutoka maeneo hayo ili tuyaokoe maisha ya watu wetu," alisema Otiende.

Kilio cha mbunge huyo kinajiri baada ya Wizara ya Afya kutangaza kuwa kaunti zinazokaribia Nairobi zinarekodi maambukizi mengi.



"Kwa siku tisa zilizopita, Nairobi imeongeza maambukizi kwa visa 5,718 vya coronavirus, Kiambu ina visa 888, Nakuru 626, Machakos 414, Kajiado 199, Nyeri 100 na Kericho 58. Idadi hizo zinajumulishwa na kuwa visa 9,893 ambavyo vinachangia maambukizi nchini," Wizara ya Afya ilisema.

Wizara hiyo imekuwa ikiwaonya Wakenya kuwa Covid-19 imelipuka katika wimbi la tatu na makali zaidi.

Wakati ugonjwa huo ulizuka mara ya kwanza Machi 2020, serikali ilichukua hatua kadhaa ikiwamo kufunga baadhi ya kaunti.



Nairobi, Mombasa na Mandera zilikuwa baadhi ya kaunti ambazo zilifungwa wakati huo na serikali ikaweka doria barabara wakazi wasiingie au kutoka maeneo hayo.

Akiongea Machi 12, Rais Uhuru aliweka masharti ya kafyu kutokuwa nje kufikia saa nne usiku pamoja na kupunguza idadi ya watu ambao wanakongama.

Alipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa nchini akitaka polisi kuwachukulia hatua kali wanaokiuka hilo.

"Hii sheria ni lazima iheshimiwe na wote. Iwe nani au nani akijaribu kukiuka atakabiliwa na sheria za taifa la Kenya inavyostahili," alisema Rais.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari kemkem za TUKO hapa

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke