Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Freeman Mbowe: Mpinzani Mkuu Tanzania augua akiwa kwenye seli

86f7fc854df7327a Freeman Mbowe: Mpinzani Mkuu Tanzania augua akiwa kwenye seli

Tue, 27 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Freeman Mbowe anakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo ya ugaidi na mauaji ya viongozi wakuu katika serikaliMbowe alikamatwa akiwa kwenye mkutano mjini Mwanza na amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Oysterbay mjini Dar es SalaamJamaa wake waliomtembelea kituoni wanasema anaugua na anatakiwa kutibiwa ila polisi hawajamruhusu kwenda hospitaliniChama cha upinzani nchini Tanzania kimedai kwamba mwenyekiti wake Freeman Mbowe ambaye alikamatwa Jumanne wiki jana ni mgonjwa na anapaswa kutibiwa.

Mbowe alikamatwa akiwa kwenye mkutano mjini mwanza na amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Oysterbay mjini Dar es Salaam.

Kwenye taarifa iliyotolewa Jumatatu, Julai 26, chama hicho kilisema kwamba kilipokea habari kutoka kwa mmoja wa jamaa wake kwamba afya ya Mbowe inaendelea kudorora.

Chama hicho kiliongezea kwamba maafisa wa polisi walikuwa wamefahamishwa kuhusu hali ya afya ya Mbowe lakini hakuna hatua ambao ilikuwa imechukuliwa.



Read also

Aliyekuwa Mbunge wa Imenti ya Kati Gideon Mwiti Amefariki Dunia

Kulingana na chama hicho wakili wa Mbowe wamesema wataamua cha kufanya iwapo serikali haitachukua jukumu la kumpeleka hospitalini kwa muda wa saa 24 zijazo.

“Tunalitaka jeshi la polisi limpeleke hospitali mara moja kwani ni haki ya mtuhumiwa kupatiwa matibabu kwa mujibu wa sheria za Tanzania," Sehemu ya taarifa za chama hicho ilisoma.

Kama ilivyoripotiwa awali na TUKO.co.ke, Mbowe alikamatwa na viongozi wengine 10 na walitupwa katika seli za kituo cha polisi cha Central mjini Mwanza.

Baada ya kukamatwa kwa Mbowe, kiongozi wa upinzani Tundu Lissu alimkashifu Rais Samia Suluhu kwa kukimya na kwamba utawala wake ulikuwa unabadilika pole pole na kufafana ule wa Hayati Rais John Pombe Magufuli.

"Wakati Rais Samia Suluhu aliingia uongozini, kulikuwa na matumaini ya uongozi mzuri, tulijua uongozi mbaya wa Magufuli umeisha na vita vya kidemokrasia vimeisha. Kukamatwa kwa mwenyekiti wa chama cha CHADEMA mheshimiwa Mbowe kumepoteza imani kwa Rais Suluhu," Lissu alisema.

Read also

Uchunguzi wa Maiti kwa Watoto 2 Aliodaiwa Kuwauwa Masten Wanjala Wafanywa

Mbowe akabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo ya ugaidi na mauaji ya viongozi wakuu katika serikali.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke