Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fisi aua mmoja na kujeruhi mwanafunzi

Fisi Aua Nguruew.jpeg Fisi aua mmoja na kujeruhi mwanafunzi

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa na kundi la fisi karibu na Chuo kimoja kikuu nje kidogo ya jiji la Nairobi.

Mmoja wa waliojeruhiwa ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Multimedia aliyeshambuliwa katika barabara moja inayopakana na Mbuga ya Taifa ya Wanyama ya Nairobi huko Ongata Rongai.

Kisa hicho kimepelekea wanafunzi kutoka chuo hicho kuandamana wakilalamikia usalama wao. Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya wanafunzi hao.

Shirika la Wanyama Pori nchini Kenya (KWS) linasema kikosi kilichotumwa kuchunguza kisa hicho kilipata sehemu za mwili wa mtu katika eneo la tukio.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live