Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fifa kuanza kujenga makao makuu ya SFF

Ad2a8aef3d8f68789b9f7fd6e8146e5f.png Fifa kuanza kujenga makao makuu ya SFF

Mon, 5 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SHIRIKISHO la Soka la Somalia (SFF) limetangaza kuwa ujenzi wa makao makuu yao na hoteli ya Mogadishu, ambavyo vinajengwa kwa mradi wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) wa `FIFA Forward Project’ unatarajia kuanza wiki hii, imeelezwa.

Wakati wa mkutano wake uliofanyika Septemba 28, 20202, Kamati ya Utendaji ya SFF ilijadaili mambo mbalimbali ya maendeleo na kutangaza kuwa ujenzi huo utaanza wiki inayoanza leo.

Kamati ya Utendaji iliishukuru Fifa kwa kuipatia Somalia mradi mkubwa kama huo, ambao utahusu ujenzi wa Makamu Makuu ya Shirikisho la Soka la Somalia na hoteli ya Mogadishu, ambayo itawapatia malazi nyota wa eneo hilo.

“Tangu kuanzishwa kwake, SFF wakati wote imekuwa katika makazi ya kupanga, lakini sasa imefikia mwisho kwa shirikisho hilo la soka kupanga. Shukrani sana Fifa kwa kutuwezesha kufanya mradi mkubwa kama huo, “ alisema Rais wa SFF na kuongeza:

“Pia tunaishukuru serikali ya Somalia kwa kuchangia sehemu ya ardhi, ambako vitajengwa Makamo Makuu ya SFF na hoteli hiyo.”

“Serikali ya Somali imetupatia sisi ardhi na baadae tuliwaomba Fifa kutupatia msaada wa fedha na kweli wameidhinisha hilo na sasa mradi huo utaanza kujengwa chini ya `Fifa Forward Project.”

MAMBO MENGINE

Mkutano huo wa Kamati ya Utendaji pia ulipanga tarehe ya kuanza kwa msimu wa mashindano ya soka wa mwaka 2020, ambayo yataanza Desemba 15. Mashindano hayo yatafanyikia kwenye Uwanja wa Mogadishu.

Timu ya Horseed Sports Club imetangazwa kuwa mwakilishi wa Somalia katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, wakati mabingwa wa sasa, Mogadishu City Club, itashiriki katika Ligi ya Mabingwa. Hii ni mwaka wapili mfululizo Somalia inashiriki mashindano ya Cafbaada ya kutokuwepo kwa karibu miongo mitatu.

Chanzo: habarileo.co.tz