Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fedha za ujenzi hospitali zapotea bila maelezo Congo DR

Drccongooo Wizara ya Afya Congo yashindwa kueleza ubadhilifu wa fedha za miradi ya afya

Tue, 14 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika lisilo la kiserikali la nchini Congo limeishutumu Mamlaka ya Afya nchini humo kwa kushindwa kueleza matumizi ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali pamoja uendeshaji wa vituo vingine vya afya.

Shirika hilo linajulikana kama' Congolese arm of the publish what you pay global network' limesema kuwa lilikagua miradi 35 kati ya 77 iliyodhaminiwa na Shirika la CFA Frans kwa dola milioni 17.2 sawa na shilingi bilioni 39.42 za kitanzania, fedha ambazo zilitolewa kwa mwaka 2019.

Aidha shirika hilo limeeleza kuwa tayari limeshakabidhi ripoti hiyo kwa Wizara ya Afya ya nchini humo wiki mbili kabla ya kuchapisha ripoti hiyo, n akueleza kuwa Wizara hiyo imekataa kujibu tuhuma hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live