Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Faranga bil 75 kutumika kuboresha huduma kwa wazee

87f8d3846cd1931a0ac3651d16fb9a70 Faranga bil 75 kutumika kuboresha huduma kwa wazee

Wed, 9 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI itatumia takriban Faranga bilioni 75 kwa miaka minne ijayo kwa huduma zinazolenga kusaidia wazee .

Kulingana na sheria ya kazi nchini Rwanda, wazee ni wale walio na umri wa zaidi ya miaka 65.

Fedha hizo zitatumika kutekeleza mpango mkakati wa kina ambao ni sehemu ya sera mpya kuhusu wazee ambayo iliidhinishwa na Baraza la Mawaziri Mei 31.

Mpango huo umegawanyika katika sehemu nne ikiwa ni pamoja na kujenga uelewa kwa wanajamii ili kuhakikisha wanajiandaa kimwili, uchumi na kisaikolojia kwa wazee kwa gharama ya takribani Faranga milioni 107 pamoja na kuboresha afya na maisha ya wazee kwa faranga bilioni 60.

Programu za nyongeza ni pamoja na kukuza maadili na mahusiano yenye Faranga milioni 673 na kuwapa wazee ulinzi na utunzaji kupitia huduma zinazofaa za msaada ambazo zimetengwa Faranga bilioni 14.

Takwimu zilizotolewa wiki iliyopita na Taasisi ya Takwimu ya Rwanda (NISR) zinaonyesha kuwa jumla ya watu 32,609 (wanaume 22,634 na wanawake 9,975) waliaga dunia mwaka 2020, kutokana na vifo vilivyotokana na magonjwa ya kuambukiza kwa asilimia 62.3, haswa wenye umri zaidi ya miaka 55.

Ingawa asilimia 87 ya wazee nchini Rwanda wamegharamiwa na Bima ya Afya ya Jamii inayojulikana kama 'Mutuelle de Santé'bado kuna changamoto mbalimbali zinazowakabii .

“Tunashukuru kwa sababu sera hii inakuja kutatua changamoto nyingi,tulikuwa tunawakilisha wazee lakini hatukuwa na nyaraka ya kuweka hoja yetu na hii ilikuwa inafanya kazi yetu ya utetezi kuwa ngumu sana lakini kuna mengi ambayo wazee wanahitaji, "alisema Mwenyekiti wa Chama cha Wastaafu Rwanda .

Chanzo: www.habarileo.co.tz