Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Familia yatoa Mil. 23 kwa aliyemrudisha kasuku aliyepotea

B1b81c2a 558a 46de 8fc1 De3543f555b6 Familia yatoa Mil. 23 kwa aliyemrudisha kasuku aliyepotea

Tue, 26 Jul 2022 Chanzo: BBC

Familia moja nchini India imetoa zawadi ya pesa taslimu ya $1,000 ambacho ni zaidi ya shilingi Mil. 23 za Kibongo kwa mtu aliyemrudisha kasuku wao aliyepotea kwa siku tano.

Rustoma, kasuku mkubwa wa Kiafrika ambaye alitawala vichwa vya habari vya India baada ya kutoroka nyumbani kwao kufuatia mlango kuachwa wazi, na familia hiyo kutangaza zawadi ya pesa taslimu kwa yeyote ambaye angemrejesha.

Rustoma aliporudishwa salama, familia yake ilikuwa na furaha sana na kutoa kiasi cha rupia 85,000 ($1,065; £885)kiasi kikubwa na zaidi ya malipo waliyokuwa wametangaza hapo awali.

Familia ya Shetty ilisema ilinunua kasuku wawili kutoka mji wa Bangalore miaka mitatu iliyopita.

Si kinyume cha sheria kuwaweka kasuku wa Kiafrika wa Kijivu kama wanyama wa majumbani India, lakini wahifadhi mara nyingi hutoa vizuizi vya kuzaliana na biashara ya ndege wa kigeni nchini India.

"Siku zote tumewachukulia kama sehemu ya familia yetu na hatujawahi kuamini kuwaweka kwenye banda," anasema Arjun Shetty, mfanyabiashara.

Anasema walipenda kuwa pamoja na ndege hao kama familia hasa Vihan, mtoto wa kiume wa Shetty mwenye umri wa miaka saba na kuiga sauti walizosikia karibu nao.

Chanzo: BBC