Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Familia yalipwa Milioni 327 na Boeing

Ethiopian Airlines Plane Crash 790 750x375 1 660x375 Familia yalipwa Milioni 327 na Boeing

Fri, 18 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Familia moja ya Kenya iliyoathirika na ajali ya Shirika la Ndege la Ethiopia ya mwaka 2019 imekubali kulipwa Shilingi milioni 327 ili kuondoa kesi dhidi ya mtengenezaji wa ndege ya Boeing ya Marekani.

Hii ni suluhu ya kwanza katika kesi waliyoshtakiwa Boeing na kutakiwa kulipa Shilingi Bilioni 109 kwa niaba ya familia nyingine ambazo zilipoteza wapendwa wao katika ajali ya Shirika la ndege la Ethiopia 737 MAX 2019 ambayo iliua watu wote 149.

Ndege hiyo iliyokuwa inaelekea Nairobi ilianguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole Addis Ababa na kuua watu 149 wakiwemo Wakenya 32.

KANISA, WANANCHI WAGOMBEA ARDHI TABATA, MVUTANO WAIBUKA

Chanzo: millardayo.com