Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Familia yakataa kuzika mwili wa Masten Wanjala kuhofia laana

Wanjala Ed.jpeg Familia yakataa kuzika mwili wa Masten Wanjala kuhofia laana

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

FAMILIA ya mshukiwa wa mauaji aliyekiri kuua watoto 10 nchini Kenya Masten Wanjala, imeukana mwili wa kijana wao wakihofia kupata laana.

Naibu Chifu wa Mukhweya Abiud Musungu alisema kuwa familia ya Wanjala ilikataa kupokea simu kutoka kwa maafisa ili wachukuliwe vipimo vya vinasaba-DNA na kumzika mtoto wao huyo wa kiume.

Chifu huyo amesema huenda serikali ikalazimika kumuua mshukiwa huyo wa mauaji iwapo familia itaendelea kuwa na msimamo wa kumkana.

Kwa upande wake,  jirani wa Wanjala, Davis Wafula, alisema kuwa kama ukoo hawakutaka kujihusisha naye kwasababu aliwaaabisha . “Tunaogopa iwapo tutamzika, sisi, kama ukoo, tunaweza kuonekana kama wauaji,” amesema jirani huyo.

Masten Wanjala alikuwa na umri wa miaka 20, alipatikana katika nyumba iliyopo katika mji wa Bungoma magharibi mwa nchi hiyo,akiwa amefariki kwa kupigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kutoroka katika Kituo cha Polisi cha Jogoo Jijini Nairobi.

Chanzo: ippmedia.com