Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Familia ya Kenei kufufua kesi ya mauaji huku ikishuku nia ya DP Ruto mazishini

0bfea400738173ed Familia ya Kenei kufufua kesi ya mauaji huku ikishuku nia ya DP Ruto mazishini

Mon, 12 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Mzee Chesang alisema licha ya Ruto kutoa ahadi wakati wa mazishi ya Kenei, sasa amekuwa anajitenga na kunyamazia suala hilo

- Mzee huyo pia alikuwa anataka kujua nia ya Ruto baada ya kutangaza mazishini kuwa maisha yake yalikuwa hatarini wakati wa kifo cha Kenei

- Kenei, ambaye alikuwa mlinzi katika ofisi ya Ruto, aliuawa mnamo Februari 21, 2020

Baba yake marehemu Kipyegon Kenei, John Chesang, ameapa kufufua kesi ya mauaji ya mwanawe huku akimuelekezea lawama Naibu Rais William Ruto.

Akizungumza na KTN News katika mahojiano Jumapili, Aprili 11, mzee Chesang alisema licha ya Ruto kutoa ahadi wakati wa mazishi ya Kenei, sasa amekuwa anajitenga na kunyamazia suala hilo.

Mzee huyo pia alikuwa anataka kujua nia ya Ruto baada ya kutangaza mazishini kuwa maisha yake yalikuwa hatarini wakati wa kifo cha Kenei na pia sababu zake za kuishtumu DCI.

"Tangu siku hiyo hakuna hatua ambayo imechukuliwa na hatujawah kuwasiliana tena. Sisi kama familia tulikuwa tunatarajia kumuona (Ruto) Kw asababu alikuwa anasema huenda yeye ndiye alikuwa analengwa badala ya Kenei. Amechukuwa hatua gani?

"Pia alikuwa anashtumu DCI. Mbona hajatufahamisha kuhusu hatua yoyote ambayo anatumia kufanya uchunguzi?Hatakai DCI na FBI anataka nini?" alimaka Chesang.



Ruto anasemakana kufanya mkutano wa faragha na familia ya Chesang na kutoa ahadi zake kwao.

Chesang pia alifichua kuwa kabla ya mauaji ya Kenei, marehemu alikuwa amejaribu kuomba uhamisho kutoka kwa ofisi ya Ruto mara mbili baada ya kushuku mgawanyiko kati ya wafanyakazi wenzake.

Baada ya kuuawa, Chesang alifahamishwa kupitia simu ya afisa mmoja mwenye hadhi ya juu kuwa Kenei alikuwa ameonywa kwamba atauawa endapo atakataa kurekodi taarifa.

Kenei, ambaye alikuwa mlinzi katika ofisi ya Ruto, aliuawa mnamo Februari 21, 2020 katika kesi ambayo Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jina ilisema ni mauaji.

Alipatikana ameuawa katika nyumba alimokuwa akiishi, katika mtaa wa Imara Daima, Nairobi.

Inadaiwa kuwa kifo chake huenda kilitokana na sakata ya utoaji zabuni feki ya ununuzi wa silaha, ya kiasi cha Sh39.4 bilioni inayomhusisha aliyekuwa Waziri wa Michezo Rashid Echesa.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke