Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Familia: CDF Ogolla alisema akifa azikwe ndani ya saa 72

(4)Generali Francis Ogola.jpeg Jenerali Francis Ogolla.

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Marehemu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Francis Ogolla wa Nchini Kenya atazikwa nyumbani kwa familia yake huko Alego Usonga, Kaunti ya Siaya siku ya Jumapili, Aprili 21, 2024.

Mwanafamilia ilifichua kuwa marehemu Jenerali Ogolla alikuwa ameeleza katika Wosia wake kwamba, atakapofariki, azikwe ndani ya saa 72.

Ogolla aliuawa katika ajali ya helikopta mnamo Alhamisi eneo la Sindar katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet, pamoja na wanajeshi wengine tisa.

Mnamo Alhamisi, Rais William Ruto alitangaza siku tatu za maombolezo kufuatia kifo cha Jenerali Francis Ogolla.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live