Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Faida ya mabenki yapungua asilimia 4

8a7e67848cc3a222de308a135076bcb1 Faida ya mabenki yapungua asilimia 4

Tue, 6 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BENKI Kuu Uganda imesema faida katika sekta ya benki imepungua kwa asilimia nne mwaka uliopita. Benki hiyo imesema faida ya sekta ya benki nchini kwa mwaka ulioishia Desemba, 2020 imepungua kwa Sh bilioni 39.3 kutokana na changamoto zilizotokana na mlipuko wa ugonjwa covid-19 ikiwamo mazuio ya shughuli za kiuchumi kwa miezi mitatu ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa huo.

Katika kipindi hicho, Benki Kuu imeonesha faida ilikuwa imepungua kutoka Sh bilioni 883.4 mwaka ulioishia Desemba 2019 hadi Sh bilioni 844.3b mwaka jana.

Takwimu za benki hiyo zinaonesha kuwa, mikopo isiyokuwa na faida kubwa ilikua hadi asilimia 5.3 hadi Desemba, 2019 kutoka asilimia 5.1 hadi Septemba, mwaka jana.

Mkurugenzi wa Utafiti katika Benki Kuu Uganda, Dk Adam Mugume alisema taasisi za kifedha zimebadilisha karibu nusu ya mikopo yao , ikiashiria athari mbaya ya covid-19 kwa uchumi.

Alisema kufikia Januari mwaka huu taasisi za kifedha zilikuwa zimebadilisha karibu nusu ya mikopo yao ambayo iliwakilisha asilimia 46 ya jumla ya mkopo yote katika sekta ya benki.

Hili lilikuwa ongezeko kutoka asilimia 40.5 Septemba, mwaka jana ambayo ilitafsiriwa hadi Sh trilioni 7.7 Aprili mwaka jana, ambapo Benki Kuu imeelekeza taasisi zote za kifedha kurekebisha mikopo yao

Chanzo: www.habarileo.co.tz