Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu ukweli wa dhana tano kuu kuhusu nyoka

Anaconda Anaconda Ball

Thu, 16 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huku Tarehe 16 mwezi Juni ikiwa ni siku ya maadhimisho ya siku ya nyoka duniani mnyama huyo hutazamwa kwa hatari kubwa, waerevu na mara nyingine hata kuhusishwa na imani potofu na uchawi katika baadhi ya jamii za Kiafrika.

Kwa kawaida nyoka anakuwa juu ya orodha ya mambo ambayo mtu anaogopa maishani mwake.

Maelfu ya watu duniani hufariki kutokana na sumu kali ya nyoka baada ya kuumwa kila mwaka kwa mujibu wa shirika la afya duniani.

Ukosefu wa matibabu na hata matibabu mabaya hufanya vifo hivyo kutokingika.

Uso kwa uso na nyoka hatari Nyoka mwenye macho matatu agunduliwa Kasisi aliyewalisha watu nyoka Afrika Kusini, afika Nigeria Sumu ya nyoka ni dawa ya kumaliza uchungu

Kuumwa na nyoka huenda kusionekane kuwa janga baya la kiafya.

Lakini katika maeneo mengine duniani ni hatari kila siku na huenda kukasababisha maafa ama hata kubadilisha maisha ya mtu.

Pengine ndio sababu ya kuwepo dhana tofuati, baadhi potofu, kuhusu wanyama hawa.

Hebu tuwafahamu zaidi. Nyoka mdogo aina ya pit viper

Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha,

Nyoka mdogo aina ya pit viper Je ni kweli?

Nyoka hawatambai kwenye mawe na kamba

Wanaweza kutambaa juu na hata chini ya mawe, kwenye miti na majengo. Nyoka hupenda kujificha ardhini.

Ni rahisi kwao kujificha chini ya vichaka, na vigumu kutambaa chini ya mawe madogo kwenye bustani.

Ni vyema kuzikata nyasi ziwe ndogo na uondoshe masalio yoyote ya nyasi zilizokatwa au majani makavu yalioangukana kujikusanya.

Kadhalika ni vymea uondoshe sehemu za mti zilizoanguka juu ya paa au zinazoning'inia kutoka nyumba yako.

Ukiona mtoto wa nyoka na familia nzima i papo

Iwapo nyoka huzaa watoto au kutaga mayai, kawaida anapojifungua huwaondokea watoto na kuwaacha kivyao.

Iwapo utamuona nyoka mkubwa karibu na mdogo basi huenda ni sadfa tu.

Wao hutawanyika punde wanapojifungua. Eyelash viper

Eyelash viper

Nyoka huteleza

Kawaida, watu ambao hawajawahi kumgusa nyoka hudhani kwamba wanyama hao huteleza ukiwagusa. Ngozi ya nyoka huonekana kuwa kavu, lakini kwa kuigusa ni nyororo.

Nyoka ni wakali

Nyoka wanaogopa binaadamu zaidi ya binaadamu wanavyowaogopa. Kwa kawaida huwa wana haya au aibu sana na iwapo wangekuwa na nafasi anaweza kutoroka asionekane.

Ni iwapo tu amekwama au ametishiwa, kama ilivyo kwa kiumbe chochote, nyoka hushambulia kujilinda.

Lakini mara nyingi baadhi huona afadhali kutoroka kuliko kushambulia.

Nyoka wote hutaga mayai

Licha ya kwamba reptilia wengi hutaga mayai, sio nyoka wote wanaotaga. Baadhi ya nyoka kama wa aina ijulikanayo kama Oriental Vine, huzaa nyoka wadogo.

Mfahamu zaidi Nyoka

Je unafahamu kwamba kuna zaidi ya aina 3000 za nyoka duniani? Kati yao, 375 wana sumu. Nchini Australia, kuna aina 140 za nyoka na 100 huwa na sumu. Nyoka mwenye sumu kali duniani ni wa Australia - Inland Taipan. Nyoka huwa na urefu wa kati ya sentimita 10 mpaka mita 7 aina ya chatu. Nyoka huishi katika mazingira tofauti ikiwemo vichaka, jangwani na hata ndani ya maji. Hutumia ulimi wao kumnusu adui kabla ya kumshambulia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live