Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu agenda kuu za Odinga iwapo atachaguliwa kuwa mwenyekiti wa AUC

Mgogoro Wa Haiti Sio Kipaumbele Cha Kenya   Odinga Fahamu agenda kuu za Odinga iwapo atachaguliwa kuwa mwenyekiti wa AUC

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchi ya Kenya hapo jana iliwasilisha rasmi ombi la Raila Odinga, kugombea nafasi ya juu katika Tume ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Maombi hayo yaliwasilishwa na katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje wa Kenya, Korir Singo’ei, ambapo pamoja na mambo mengine, yalijumuisha mikakati ya Odinga ikiwa atachaguliwa kama mkuu wa kamisheni ya AU.

Miongoni mwa mambo ambayo Odinga amesema yalimsukuma kugombea nafasi hiyo, ni pamoja utangamano wa Afrika, maendeleo ya miundombinu, ukombozi wa kiuchumi wa barra hilo, kujitegemea kwa mataifa na kuhamasisha biashara huria barani Afrika.

Maeneo mengine ni kilimo, amani na usalama pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kuwasilishwa kwa maombi ya Odinga, kunamaliza rasmi wasiwasi uliokuwepo kuhusu utayari wa Serikali kumsaidia, hasa baada ya msimamo wake wa hivi karibuni kuhusu maandamano ya vijana wa Gen Z nchini humo.

Odinga anatarajiwa kushindana na wagombea wengine ambao ni waziri wa mambo ya nje wa Djibouti, Mahmoud Ali Youssouf, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Somalia, Fawzia Yusuf Adam na makamu wa rais wa zamani wa Ushelisheli, Vincent Meriton.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live