Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Facebook yamkutanisha na baba ake baada ya miaka 27

0857023279af2591 Facebook yamkutanisha na baba ake baada ya miaka 27

Thu, 12 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Getrude alisema alilelewa na babu yake na bibi na hivyo hakuwa na hamu ya kumtafuta baba yake Ilikuwa baada ya kifo cha babu ndipo aliamua kumtafuta baba yakeHata hivyo, alikutana na kwenye Facebook baada ya kusubiri kwa muda mrefu akimtafutaMrembo Mkenya ameibua hisia mseto mitandaoni baada ya kusimulia namna alikutana na baba yake kwa mara ya kwanza kupitia Facebook.

Getrude Wanjiru alifichua kwamba hakuwa anamfahamu baba yake kwa miaka 27, hadi alipomtafuta kwenye Facebook.

Akizungumza katika mahojiano na NTV, Wanjiru alisema alilelewa na babu na bibi yake.

''Mama yangu alinizaa na kunipeleka kwa wazazi wake," Getrude alisema.

Getrude alisema hakuwa na hamu ya kumtafuta baba yake kwa sababu babu yake alikuwa amejitwika wajibu huo.

"Sikushughulika kumtafuta baba yangu kwa sababu alikuwa babu yangu alikuwa kama baba kwangu na alinipa chochote nilichokuwa nataka," alisema

Ilikuwa baada ya kifo cha babu akiwa katika chuo kikuu ndipo aliamua kumtafuta baba yake kujaza pengo hiyo.



"Wakati babu yangu alifariki, nilimuuliza mama yang kumhusu baba yangu lakini hakuniambia chochote. Kwa hivyo nilisoma hadi nikamaliza chuo kikuu mwaka 2016," Getrude aliongezea.

Hofu ya kuchumbiana na jamaa wakeAlisisitiza kuwa alikuwa anahofia kuingia katika mahusiano ya kimapenzi akiwa na hofu kuwa huenda atachumbiana na baba yake ama kaka zake bila kujua na hivyo alimshinikiza mama yake amuonyeshe baba yake.

Hatimaye mwaka 2019, mama yake aliamua kumuambia kumhusu baba yake pamoja na jina lake japo hakuwa na nambari zake za simu.

Hivyo Getrude aliamua kufanya utafiti wa kumsaka baba yake.

Msako wake ulianzia Facebook, na kwa bahati nzuri alimpata baba yake na mama yake alimthibitishia kuwa kweli jamaa huyo alikuwa baba yake mzazi.

Hata hivyo, mzee huyo mara ya kwanza alikataa kuamini lakini hatimaye alichukuwa hatua ambayo ilimfurahisha Getrude.

Getrude alisema alifurahi wakati baba yake aliwasiliana naye na hata kupanga wakutane.

Watoto waliotupwa waokolewaKatika taarifa tofauti ya TUKO.co.ke, wasamaria wema waliwaokoa watoto watatu ambao baba yao alikuwa amefungwa jela.



Norman, Kibiwott, na Meshack ni wenye umri wa kati ya 12 na saba na wamekuwa wakiihsia peke yao bila wazazi.

Kulingana na chifu wa eneo hilo Moses Keitany, baba ya watoto hao Timothy Kimutai amefungwa jela na haijulikani atawachiliwa huru lini.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke