Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FIFA yafuta mchezo wa Guinea vs Morocco kutokana na hali usalama

Moricco Kikosi cha Timu ya Taifa ya Morocco

Mon, 6 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la soka ulimwenguni (FIFA) limefuta Mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 Qatar kati ya Guinea vs Morocco iliyokua ichezwe leo nchini Guinea kutokana na machafuko ya kisiasa nchini .

Hali ya Usalama nchini Guinea si nzuri baada ya Jeshi la nchi hiyo kuvamia Ikulu na kutangaza kumpindua Rais Alpha Conde na kumuweka chini ya ulinzi.

Kufuatia tukio hilo FIFA imeufutilia mbali mchezo huo uliokuwa upigwe nchini Guinea kwa kuwa hakuna Usalama, huku katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo kukitolewa taarifa ya kutotembea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live