Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

FCC: Tshisekedi amevuruga uchaguzi

Tshisekedi Aonya Mtafaruku Wa Maaskofu Rais anayetetea kiti chake DR Kongo Felix Tshisekedi

Fri, 22 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama hicho cha rais wa zamani Joseph Kabila, ambacho kilisusia mchakato wa uchaguzi, "kinadai Rais Tshisekedi na washirika wake katika Tume ya Uchaguzi CENI walipanga na kuhusika na vurugu hizo.

Msimamo huu unafuatia ule wa wagombea watano wa Urais akiwemo Martin Fayulu na Denis Mukwege waliotaka uchaguzi uandaliwe upya na tume ya uchaguzi itakayo ridhiwa na pande zote.

Wakati huohuo CENI imeagiza kuendelea kwa uchaguzi Leo Alhamisi (21.12.2023) katika vituo ambavyo zoezi hilo halikufanyika hapo jana.

Wapiga kura wanamchagua rais, wabunge na wajumbe wa serikali za mitaa. Rais aliyoko madarakani Felix Tshisekedi, anagombea muhula wa pili. Upigaji kura ulicheleweshwa kwa kiwango kikubwa hapo jana, nchini kote.

Majina yakosekana kwenye daftari

Matazizo mengi yalitokea pale wapiga kura walipokosa kuona majina yao kwenye daftari la kupigia kura.

Mjini Kinshasa vituo vya kupigia kura vilibaki wazi hadi saa tano usiku. Tume ya uchaguzi ililaumiwa kwa matatizo ya kiufundi yaliyotokea. Baadhi ya raia wanasema licha ya dola bilioni moja na laki mbili milioni ilishindwa kuaanda uchaguzi unaoaminika.

Kongo ni takriban mara nne ya ukubwa wa Ufaransa, lakini haina miundombinu ya kimsingi - hata baadhi ya miji yake kuu haijaunganishwa na barabara. Umoja wa Mataifa, Misri na nchi jirani ya Kongo-Brazzaville zilisaidia kusafirisha nyenzo za uchaguzi katika maeneo ya mbali. Lakini hata hivyo bado kunamaeneo ambayo vifaa vya uchaguzi bado kuwasili.

Watu milioni 44 wamejiandikisha kupiga kura katika nchi hiyo yenye jumla ya watu milioni 100.  Matokeo ya uchaguzi yatatangazwa baada ya siku kadhaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live