Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Etienne:Nawafatilia wapinzani wangu

Taifa+starss+pic Etienne:Nawafatilia wapinzani wangu

Tue, 6 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By THOMAS NG'ITU NA RAMADHAN ELIASKOCHA mkuu wa timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars', Etienne Ndayiragije ameweka wazi kwamba anawafahamu wapinzani wake ambao atakutana nao katika hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa Afrika na Kombe la Dunia.

 "Nawafatilia Tunisia kwa ukaribu na najua kwamba tarehe 13 wanacheza mchezo wa kirafiki na Nigeria, najua kabisa wakiwa nyumbani wanakuwa bora zaidi, pia timu hii ina wachezaji wengi wanaocheza Ligi ya kwao, wanatoka mara moja kwenda nje ya nchi yao lakini wanarudi tena kwao" amesema Ndayiragije.

 Akizungumzia upande wa wachezaji ambao amewaita lakini wadau wamekuwa wakihoji sana amesema yeye anaamini kabisa kwamba watafanya kitu  kikubwa katika kikosi chake.

 "Mfano niliwahi kumuita Nchimbi walihoji lakini ni mchezaji mwenye nguvu, mbio na anajua kuficha mpira, hii pia ni mechi ya kirafiki nimeita hawa, pia kuna wachezaji kama watano walinipigia simu wakaniuliza kwanini sijawaita nikawaambia wanifanyie kazi kwa sababu bado kuna CHAN" amesema.

AFICHUA MAOVU YA KLABU ZA LIGI KUU

Etienne alisema wakati wa mazoezi amekuwa akitembelea viwanja mbalimbali vya mazoezi ambapo timu za Ligi Kuu huwa wanafanya mazoezi, ameona Simba ndio timu pekee ambayo inakuwa inataka magoli kwni imekuwa ikiwafundisha  wachezaji  wake kufunga.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz