Tangu kuanza kwa mzozo wa Tigray Novemba 2020, Mamlaka za Serikali zimetumia mwanya huo kuwazimia Huduma ya Intaneti Wakazi wa eneo hilo kwa zaidi ya Siku 300 sasa
Kukosekana kwa Huduma hiyo kumesababisha Matukio mengi ya Ukiukwaji wa Haki Za Binadamu kushindwa kurekodiwa ikiwemo Ubakaji, Unyanyasaji wa Kijinsia na Ukatili unaofanywa kwa Wakimbizi.
Mzozo katika Jimbo la Tigray ulianza Novemba 4, 2020, ambapo serikali na jeshi la shirikisho, likisaidiwa na wanamgambo, vikosi vya jeshi na vikosi maalum vya jimbo hilo, kuanza kukabiliana na waasi wa Tigray wa TPLF, chama cha zamani kilichoongoza Ethiopia kuanzia mwaka wa 1991 hadi 2018.