Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia yawatimua maafisa wa UN kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi

Ethiopia Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Fri, 1 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ethiopia imewapa maafisa 7 wakuu wa Umoja wa Mataifa (UN) muda wa saa 72 kuondoka nchini humo "kwa kujihusisha na maswala ya ndani ya nchi", ujumbe wa Tweeter kutoka kwa wizara ya mambo ya nje unasema.

Maafisa hao ni pamoja na wakuu wa shirika la watoto la Umoja wa Mataifa Unicef, Adele Khodr, na kaimu mkuu wa ofisi ya masuala ya binadamu Grant Leaity,UNOCHA.

Umoja wa Mataifa umehusika sana katika juhudi za kujaribu kufikisha misaada katika eneo la Tigray linalokumbwa na mapigano. Inakadiria kuwa zaidi ya watu milioni tano kaskazini wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Umoja wa Mataifa (UN) imeelezea kushtushwa kwake na hatua ya Ethiopia kuwafukuza nchini humo maafisa wake wakuu.

Hii ni baada ya Ethiopia kuwapa maafisa saba wakuu wa Umoja huo muda wa saa 72 kuondoka nchini humo "kwa kujihusisha na maswala ya ndani ya nchi", ujumbe wa Tweeter kutoka kwa wizara ya mambo ya nje unasema.

Maafisa hao ni pamoja na wakuu wa shirika la watoto la Umoja wa Mataifa Unicef, Adele Khodr, na kaimu mkuu wa ofisi ya masuala ya binadamu Grant Leaity,UNOCHA.

Umoja wa Mataifa umehusika sana katika juhudi za kujaribu kufikisha misaada katika eneo la Tigray linalokumbwa na mapigano. Inakadiria kuwa zaidi ya watu milioni tano kaskazini wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live