Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia yawarejesha nyumbani watu 455,000 waliokimbia makazi yao

Ethiopia Kuanza Tena Kuwarejesha Makwao Raia Wake Kutoka Saudi Arabia Ethiopia yawarejesha nyumbani watu 455,000 waliokimbia makazi yao

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Ethiopia imetangaza kuwa imefanikiwa kuwarejesha makwao wakimbizi wa ndani 455,449 (IDPs) katika kipindi cha miaka michache iliyopita.

Shirika la Habari la Ethiopia limemnukuu Abdulaziz Mohammed, mkuu wa Tume ya Kudhibiti Maafa na Hatari ya Jimbo la Benishangul-Gumuz akisema kuwa, wakimbizi 455,449 kati ya wakimbizi wa ndani (IDPs) 475,380 wa eneo hilo wameweza kurejea mwakao katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni.

Aidha amesema: "Wakimbizi hao walikimbia maeneo yao kutokana na mchanganyiko wa majanga ya kimaumbile na yale yaliyosababishwa na binadamu ambayo yaliathiri sehemu kubwa za eneo la magharibi mwa Ethiopia." Bwawa la al Nahdha

Afisa huyo mwandamizi wa masuala ya kudhibiti maafa nchini Ethiopia pia amesema kuwa, uongozi wa mkoa wake unawasaidia wakimbizi waliorejea makwao kupata nafasi mpya za kazi ikiwa ni pamoja na kwenye sekta ya kilimo.

Katika miaka ya hivi karibuni, ghasia baina ya jamii mbalimbali na mashambulizi ya waasi yamesababisha vifo vya maelfu ya raia na mamia kwa maelfu ya watu kuhama makazi yao huko magharibi mwa Ethiopia.

Eneo la Benishangul-Gumuz, lililoko kaskazini-magharibi mwa Ethiopia na ambalo linapakana na Sudan, ndiko liliko Bwawa Kuu la al Nahdha (Renaissance) la Ethiopia lenye uwezo wa kuzalisha megawati 5,150 za umeme. Bwawa hilo ndio mtambo mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme kwa maji barani Afrika ingawa bado linaendelea kujengwa na halijakamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live