Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia yateua timu ya mazungumzo eneo la waasi wa Tigray

Abiy Pic Abiy Ahmed, Waziri Mkuu Ethiopia

Wed, 29 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu hiyo itaongozwa na Naibu Waziri Mkuu Demeke Mekonnen. Wajumbe wengine ni Waziri wa Sheria Gedion Timothewos, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Temesgen Tiruneh, Balozi Redwan Hussein, mshauri wa masuala ya usalama wa Waziri Mkuu Lt-Jenerali Berhanu Bekele, Balozi Hassan Abdulkadir na Dk Getachew Jember.

Dk Gedion alisema chama kitafuata "amani kwa njia inayoheshimu katiba na maslahi ya taifa,” kwa kuwezeshwa na Umoja wa Afrika.

Hakukuwa na maoni yoyote ya haraka kutoka kwa viongozi wa waasi wa Tigray juu ya tangazo hilo.

Wakati wa kikao cha bunge mnamo Juni 14, Waziri Mkuu, Abiy Ahmed alitangaza kwamba serikali yake imeunda timu ya kujadiliana na waasi wa Tigray katika jitihada za kumaliza mgogoro wa umwagaji damu uliodumu kwa miezi 18 kaskazini mwa nchi hiyo.

Katika kujibu, chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF) kilisema kiko tayari kwa "mchakato wa amani unaoaminika, usio na upendeleo na wenye kanuni ambao unashirikisha wahusika kwa umakini, unaojumuisha na unaozingatiwa."

Rais wa eneo la Tigray na kiongozi wa TPLF Debretsion Gebremichael alisema watatuma ujumbe wa ngazi ya juu kwenye mazungumzo yatakayoitishwa na kusimamiwa na serikali ya Kenya.

Mzozo huo uliozuka huko Tigray mnamo Novemba 2020, umegharimu maisha ya maelfu ya watu na kusababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu, na kusababisha asilimia 90 ya watu wa Tigrayan kuishi katika hali ya njaa.

Makubaliano ya pande zinazozozana kufanya mazungumzo ya moja kwa moja yamefungua dirisha la matumaini ya kumalizika vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live