Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia yasitisha mapigano na Tigray

56881514 303 660x394.jpeg Ethiopia yasitisha mapigano na Tigray

Tue, 29 Jun 2021 Chanzo: millardayo.com

Serikali ya Ethiopia imetangaza sitisho la mapigano katika jimbo la Tigray, miezi minane baada ya mzozo mbaya uliosababisha mafaa mengi, wakati maelfu ya wakazi wakikabiliwa na baa la njaa.

Sitisho hilo la mapigano huenda likatuliza hali kwenye taifa hilo la pili kwa wingi wa watu barani Afrika.

Taarifa inajiri wakati Ethiopia ikisuburi matokeo ya uchaguzi wa kitaifa ambao Waziri Mkuu Abiy Ahmed aliuelezea kama kiini cha mageuzi yaliyompelekea kushinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2019.

Taarifa ya Serikali ilitolewa na vyombo vya habari muda mfupi baada ya utawala wa mpito wa Tigray ulioteuliwa na serikali kuu kukimbia katika Mji Mkuu wa Tigray, Mekele, na kuomba sitisho la mapigano kwa sababu za kibinadamu ili misaada inayohitajika ifikishwe kwa kwa wakazi.

Wakati huo huo, wakazi wa Mekele wameshangilia kuwasili kwa vikosi vya Tigray.

POLISI WATEMBEZA KICHAPO NJE YA UWANJA, MASHABIKI WAKILAZIMISHA KUINGIA UWANJANI

Chanzo: millardayo.com