Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia yaripoti uwepo wa Kirusi cha Dellta

Delta Ethioia Ethiopia yaripoti uwepo wa Kirusi Delta

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Afya nchini Ethiopia imeripoti kwa mara ya kwanza uwepo wa ugonjwa UVIKO-19 unaosababishwa na Kirusi kipya cha Delta.

Taarifa hii imetolewana Waziri wa Afya wa nchini humo,Dk.Lia Tadesse huku akiwataka wanachi wote kuchukua tahadhari za kujikinga dhidi ya ugonjwa huo kwa kufuata maelekezo yanayotelewa na Wizara hiyo.

Hata hivyo taarifa hiyo haijaweka wazi idadi ya watu walioathirikia na virusi hivyo, bali ilibainisha juu ya kuongezeka kwa wagonjwa pamoja vifo vinavyotokana na virusi hivyo.

Wiki kadhaa zilizopita, Waziri huyo alitangaza kuwa timu ya utafiti kutoka Wizara hiyo inafatilia kujua kama tayari Virusi vya Delta vimesambaa nchini humo, na ripoti ya timu hiyo ilionesha uwepo wa visa vipatavyo 300,000 vya UVIKO-19 visivyo sababishwa na Delta, pamoja na vifo zaidi ya 4,000 huku idadi ya waliopona kuwa zaidi ya 200,000.

Hata hivyo Wizara hiyo imeendelea kusisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kuchomachanjo ya UVIKO-19 ili kuweza kupambana na janga hilo la kidunia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live