Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia yapiga marufuku watu kutoka nje usiku baada ya watu kuuawa

Ethiopia Yapiga Marufuku Watu Kutoka Nje Usiku Baada Ya Watu Kuuawa Ethiopia yapiga marufuku watu kutoka nje usiku baada ya watu kuuawa

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Mamlaka katika eneo la magharibi mwa Ethiopia la Gambella imeweka marufuku ya kutotoka nje usiku baada ya watu wengi kuuawa katika ghasia zilizoanza upya.

Amri ya kutotoka nje - ambayo inaanza kutekelezwa mara moja - inakataza harakati za magari na mtu binafsi kati ya 7pm na 6am.

Serikali ya eneo haijataja takwimu za majeruhi lakini iliapa katika taarifa yake kuwawajibisha "wajumbe wa uongozi" ambao ilisema walihusika katika "uvurugaji wa amani."

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani ghasia hizo zilianza mapema wiki hii na zimekuwa na mwelekeo wa kikabila huku takriban maeneo mawili yakishuhudia mapigano.

Vyanzo vya habari katika mji mkuu wa mkoa wa Gambella vilisema biashara na ofisi zilifungwa siku ya Jumatano.

Eneo hilo ambalo linapakana na nchi jirani ya Sudan Kusini, limeshuhudia vurugu za mara kwa mara katika miezi ya hivi karibuni.

Mwezi Mei takriban watu saba waliripotiwa kuuawa huku makumi ya wengine wakijeruhiwa katika mapigano katika mji mkuu wakati mwaka jana mji huo ulivamiwa na wapiganaji waasi kutoka mkoa jirani wa Oromia ambapo makumi ya watu waliuawa.

Chanzo: Bbc