Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia yakamilisha kujaza maji bwawa lenye utata Mto Nile

Ethiopia Yakamilisha Kujaza Maji Bwawa Lenye Utata Mto Nile Ethiopia yakamilisha kujaza maji bwawa lenye utata Mto Nile

Sun, 10 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Ethiopia inasema imekamilisha awamu yake ya nne na ya mwisho ya kujaza maji bwawa kubwa lenye utata katika eneo la Blue Nile.

Tangazo hilo lilitolewa leo Jumapili, wiki kadhaa baada ya mazungumzo kati ya Addis Ababa na nchi mbili zinazonufaika na mto Nile- Misri na Sudan. Mazungumzo yalianza tena kwa nia ya kutia saini makubaliano yenye nguvu ya kukabiliana na ukame katika siku zijazo.

Duru mpya ya mazungumzo inatarajiwa kufanyika mwezi huu wa Septemba.

Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD) lenye thamani ya dola bilioni 5 limekuwa katikati ya mazungumzo ya kidiplomasia katika muongo mmoja uliopita- kati ya Ethiopia na nchi hizo mbili ambazo zinahofia kwamba upatikanaji wao muhimu wa maji kupitia mto Nile unaweza kutishiwa au kuathiriwa na mradi huo.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani wa Twitter) Waziri Mkuu Abiy Ahmed alisifu kukamilika kwa ujazo huo kama hatua kubwa ambayo ilifanyika licha ya "changamoto za ndani na shinikizo kutoka nje."

Habari hizo zinakuja huku kukiwa na ghasia zinazoendelea na kuongezeka kwa ukosefu wa usalama katika maeneo mengi kote nchini Ethiopia- nchi ambayo bado inakabiliwa na makovu ya vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka miwili, vilivyomalizika mwaka jana kwa makubaliano ya amani.

Chanzo: Bbc