Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia yaja na mbinu hii kumaliza mapigano Tigray

Abiy Pic Abiy Ahmed, Waziri Mkuu Ethiopia

Wed, 15 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema serikali imeunda kamati ya kufanya mazungumzo na vikosi vya Harakati ya Ukombizi wa Watu wa Tigray (TPLF).

Abiy Ahmed alisema hayo jana Jumanne akilihutubia Bunge la nchi hiyo na kufafanua kuwa: Kuhusu amani, kuna kamati imebuniwa. Mazungumzo yanahitaji kazi kubwa. Kamati hiyo iliyoundwa itathmini namna tutakavyofanya mazunugumzo hayo.

Tarehe 25 Machi mwaka huu, serikali ya Ethiopia ilitangaza usitishaji vita wa upande mmoja ikisema kuwa utasaidia misaada ya kibinadamu kuelekea Tigray.

Wapiganaji wa Tigray pia walikubali kuheshimu usitishaji vita huo kwa sharti kwamba misaada ya kutosha itumwe katika eneo hilo katika muda mwafaka.

Tangu mwezi Novemba mwaka juzi eneo la Tigray limekumbwa na hitilafu na mivutano ya kisiasa kati ya serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed na viongozi wa eneo hilo ambao wakati fulani waliongoza serikali ya Ethiopia.

Vita vilivyoshuhudiwa katika eneo hilo hadi sasa vimesababisha kuuliwa makumi ya maelfu ya watu na kupelekea mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live