Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia yaishutumu Misri kuingiza siasa kesi Bwawa la Renaissance

Nile Egypt Ethiopia yaishutumu Misri kuingiza siasa kesi ya Bwawa la Renaissance

Thu, 13 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ethiopia ameishutumu Misri kwa kujaribu kuingiza siasa katika suala la Bwawa la Renaissance na maji ya Mto Nile.

Kwa mujibu wa ripoti ya kituo cha habari cha Russia Today, Mesganu Arga, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, amesema katika kikao chake na Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, kwamba: Tuna msimamo thabiti juu ya haja ya kuendelea na mazungumzo na Misri na Sudan kuhusu Bwawa la Renaissance chini ya usimamizi wa Umoja wa Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia ameishutumu Misri kwa kujaribu kuingiza siasa katika suala la Bwawa la Renaissance na maji ya Mto Nile na kusema: Juhudi hizo hazina maslahi kwa upande wowote.

Ethiopia ilianza kuzalisha umeme kutoka kwenye Bwawa la Renaissance mnamo Februari 2022.

Mnamo Agosti 2022, hatua ya tatu ya kujaza maji katika bwawa hilo pia ilikamilishwa, na hatua ya nne imepangwa kuanza katika msimu wa joto.

Ujenzi wa Bwawa la Renaissance juu ya maji ya Mto Nile huko Ethiopia umeibua mvutano mkubwa wa maji kati ya nchi tatu za Misri, Sudan na Ethiopia tangu mwaka 2011 hadi sasa. Misri na Sudan, ambazo zote mbili ni nchi za juu katika Bonde la Mto Nile zinazotegemea sana mto huo kwa mahitaji ya maji safi, zina wasiwasi kuwa bwawa hilo linaweza kuathiri rasilimali zao za maji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live