Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia yaipa leseni kampuni ya simu ya Kenya

Ethiopia Yaipa Leseni Kampuni Ya Simu Ya Kenya Ethiopia yatoa leseni huduma ya pesa kwa njia simu kwa kampuni ya Kenya

Thu, 11 May 2023 Chanzo: Bbc

Ethiopia imeipatia kampuni kubwa ya mawasiliano ya Safaricom leseni ya kuendesha huduma za pesa kwa simu, kampuni ya kwanza ya kigeni kupata kibali kama hicho katika taifa hilo lenye watu wengi.

Safaricom ilizinduliwa mwezi Agosti mwaka jana shughuli zake nchini Ethiopia, ambayo kwa miaka mingi imekuwa mojawapo ya soko kubwa lililofungwa katika bara la Afrika.

Kampuni ya simu ya Ethio inayomilikiwa na serikali ilikuwa mtoa huduma pekee wa huduma za mawasiliano ya simu na simu kwa nchi yenye zaidi ya watu milioni 110.

Lakini Addis Ababa ilifungua soko lake mwaka wa 2021 kwa wazabuni wa kimataifa, na kuupa muungano unaoongozwa na Safaricom leseni ya kufanya kazi nchini humo.

Siku ya Alhamisi, Benki ya Kitaifa ya Ethiopia (NBE) ilisema katika taarifa kwamba utoaji wa leseni ya pesa kwa njia ya simu uliakisi malengo yake yanayoendelea ya "kukuza uvumbuzi wa kifedha na kujumuishwa katika soko la Ethiopia".

Afisa mkuu mtendaji wa Safaricom Peter Ndegwa alisema kampuni hiyo itasambaza huduma za kifedha kwa njia ya simu nchini kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Ethiopia imeshuhudia ukuaji mkubwa wa huduma za pesa kwa simu katika miezi ya hivi karibuni.

Wiki mbili zilizopita, mamlaka ilianzisha huduma ya pesa kwa njia ya simu kuwa njia pekee ya malipo katika vituo vya mafuta na taasisi za kifedha za serikali kwa nia ya kuwavuta watu kwenye malipo ya kidijitali.

Chanzo: Bbc