Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia yaapa kutatua mzozo ulioua watu 100,000

Bw Abiy Ethiopia yaapa kutatua mzozo ulioua watu 100,000

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa ulinzi wa Ethiopia Abraham Belay ametangaza mipango ya kura ya maoni juu ya hakikisho kwamba migogoro ya maeneo ya Tigray na Amhara itatatuliwa kwa kuzingatia sheria ya kikatiba na kwa mujibu wa mkataba wa amani uliotiwa saini mwezi Novemba mwaka jana.

Waziri Belay ameashiria Mkataba wa Pretoria na malalamiko ya wakaazi na zaidi ya watu milioni 2.5 waliokimbia makazi yao kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka miwili huko Tigray na kusema, “Tunajitahidi kwa dhati kutatua masuala ambayo yamepuuzwa na kusababisha madhara makubwa kwa watu wetu. Wakaazi wa maeneo haya pia watahakikishiwa msingi thabiti wa kuwachagua na kuwasimamia magavana wao."

Eneo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray lilikumbwa na vita vikali mwaka 2020, ambavyo vilimalizika Novemba mwaka jana baada ya serikali ya shirikisho na chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF) kutia saini Mkataba wa Pretoria, mkataba wa amani unaosimamiwa na Umoja wa Afrika uliotiwa saini katika mji mkuu wa Afrika Kusini.

Taasisi ya Utafiti wa Amani ya Oslo (PRIO) iliainisha Vita vya Tigray kama mzozo mbaya zaidi ulimwenguni mnamo 2022, ambapo watu zaidi ya 100,000 waliripotiwa kupoteza maisha katika mgogro huo. Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Kulingana na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa zaidi ya watu milioni 2.6 wamekimbia makazi yao kutokana na mzozo huo ambapo pia umeibua uhaba mkubwa wa chakula.

Mapema mwezi huu, mapigano makali yalizuka kati ya Jeshi la Ethiopia (ENDF) na wanamgambo wa eneo la Fano wa Amhara juu ya uamuzi wa serikali wa kuunganisha vikosi vya kikanda katika polisi wa shirikisho au jeshi.

Serikali ilitangaza hali ya hatari ya miezi sita wiki iliyopita ili kukabiliana na ghasia zilizotokea Bahir Dar, Gondar, mji wa kihistoria wa Lalibela na miji mingine, ambazo zimesababisha vifo vya raia kadhaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live