Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia yaahirisha uchaguzi katika Majimbo mawili

Screenshot 2021 06 11 At 17.06.51 660x400.png Ethiopia yaahirisha uchaguzi katika Majimbo mawili

Sat, 12 Jun 2021 Chanzo: millardayo.com

Tume ya uchaguzi ya Ethiopia imeahirisha kufanyika uchaguzi hadi mwezi wa Septemba katika majimbo mawili ya Somali na Harari.

Upigaji kura uliyotarajiwa kufanyika katika muda wa siku 10 zijazo hautafanyika pia katika jimbo la Tigray ambako kuna mzozo unaoendelea kwa wakati huu.

Maafisa wa uchaguzi wanasema kasoro za upigaji kura na matatizo ya kuchapisha vyeti vya kura yamesababisha kucheleweshwa kufanyika uchaguzi huo.

Shirika la habari la Uingereza, Reuters limemnukuu mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Birtukan Mideksa akisema kwamba katika baadhi ya wilaya uchaguzi utafanyika mnamo duru ya pili hapo Septemba 6.

Hakuna tarehe iliyotajwa kwa ajili ya uchaguzi wa Tigray. Uchaguzi mkuu ulipangwa kufanyika mwezi Agosti mwaka 2020, lakini uliahirishwa kutokana na janga la virusi vya corona

MKE WA TB JOSHUA AFICHUA MWANZO MWISHO ALIVYOFARIKI, ALIOGA, IBADANI, AKAFIA CHUMBA MAALUM

Chanzo: millardayo.com