Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia wahusishwa na kashfa ya udanganyifu, wanyimwa msaada

Ethiopia Wahusishwa Na Kashfa Ya Udanganyifu, Wanyimwa Msaada Ethiopia wahusishwa na kashfa ya udanganyifu, wanyimwa msaada

Fri, 16 Jun 2023 Chanzo: Voa

Shirika la misaada ya kibinadamu la serikali ya Marekani, na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) walitangaza kuwa wanasitisha msaada wa chakula kwa eneo la Tigray lililokumbwa na vita nchini Ethiopia, baada ya kugundua kuwa shehena zilipelekwa katika masoko ya ndani.

Viongozi katika serikali ya Ethiopia na mashirika ya misaada ya kibinadamu ni miongoni mwa washukiwa 186 wanaohusishwa na kashfa ya udanganyifu katika usambazaji, wa misaada ya chakula iliyokusudiwa kwa ajili ya kaskazini mwa nchi hiyo, tume ya uchunguzi ya Tigray imesema Alhamisi.

Mapema mwezi Mei, shirika la misaada ya kibinadamu la serikali ya Marekani, na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) walitangaza kuwa wanasitisha msaada wa chakula kwa eneo la Tigray lililokumbwa na vita nchini Ethiopia, baada ya kugundua kuwa shehena zilipelekwa katika masoko ya ndani.

Siku chache baadaye mashirika yote mawili yaliongeza uamuzi huo kwa Ethiopia nzima, huku USAID ikitaja kampeni iliyoenea na iliyoratibiwa ya kugeuza vifaa vilivyotolewa kutoka kwa wahitaji kama sababu ya kusimamishwa kwa shughuli hiyo.

Kulingana na Fiseha Kidanu, mkuu wa uchunguzi ulioanzishwa na mamlaka ya Tigray, mashirika matano ikiwemo serikali ya Eritrea, serikali ya Ethiopia, mamlaka ya mkoa wa Tigray, waratibu wa kambi za watu waliohamishwa na wafanyakazi wa misaada, walishiriki katika udanganyifu huo, vyombo vya habari rasmi viliripoti.

Chanzo: Voa