Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia na Sudan zasusia mkutano wa Jumuiya ya IGAD

IGAD Sudan Ethiopia na Sudan zasusia mkutano wa Jumuiya ya IGAD

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ethiopia imesema mkutano wa Wakuu Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali (IGAD) umefanyika leo Alhamisi huku ikiwa na mipango mengine. Wakati huo huo Sudan pia imedai kuwa haikushirikishwa katika ajenda ya mkutano huo.

Mivutano imeongezeka ndani ya jumuiya ya kikanda ya IGAD, kufuatia baadhi ya nchi wanachama wake kuonyesha waziwazi kutokua na imani na taasisi hiyo ya kikanda.

IGAD inazijumuisha nchi za Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Sudan na Uganda. Jumuiya ya kikanda ya IGAD

Mapema wanachama wawili wa IGAD wameweka wazi kwamba hawatahudhuria Mkutano wa leo wa Wakuu wa nchi wa jumuiya ya IGAD. Mkutano huo ulitazamia kuyapatia ufumbuzi masuala ya msingi yanayozikabili nchi nchi wanachama.

Ethiopia kwa upande wake imesema kuwa haitaweza kuhudhuria mkutano huo ikisema kuwa yapo baadhi ya mambo yanayouingilia mkutano huu tajwa.

Djibouti, ambayo ni Mwenyekiti wa jumuiya ya IGAD, tarehe 11 Januari 2024 ilitoa mualiko kwa nchi wanachama kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa leo wa Wakuu wa jumuiya hiyo ya kikanda.

Mwaliko huo ulieleza kuwa mkutano wa Alhamisi ya leo utajikita katika "masuala mawili makuu ambayo ni masuala yanayoendelea kati ya Jamhuri ya Shirikisho la Ethiopia na Jamhuri ya Shirikisho la Somalia na hali ya mambo huko Sudan."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live