Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia kuzifunga Balozi zake zilizopo Misri na Ireland

CLOSEDGG Abiy Ahmed, Waziri Mkuu Ethiopia

Tue, 28 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ethiopia imelazimika kuzifunga Balozi zake zilizopo nchini Misri pamoja na Ireland kufuatia kuporomoka kwa uchumi wa taifa hilo uliosababishwa na mgogoro wa muda mrefu uliopo katika mkoa wa Tigray.

Balozi wa Ethiopia nchini Misri, Markos Tekle, ametangaza kuwa ubalozi wa nchini hiyo uliopo katika Mji Mkuu wa Cairo utafungwa kwa muda ifikapo mwezi Oktoba "Ubalozi huu utafungwa kwa miezi mitatu hadi sita ijayo ili kupunguza gharama na matumizi" Amesema Balozi huyo.

Aidha amefafanua kuwa maamuzi ya kuufunga Ubalozi huo hayajatokana na mzozo uliopo baina ya mataifa hayo mawili pamoja na Sudan kuhusu Bwawa (Grand Ethiopian Renaissance Dam GERD) lililopo nchini Ethiopia.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa sababu za kufunga Ubalozi wake uliopo katika mji wa Dublin nchini Ireland ni zinafafana na zile za Misri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live