Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia kuwarejesha makwao raia wake kutoka Saudi Arabia

Ethiopia Kuanza Tena Kuwarejesha Makwao Raia Wake Kutoka Saudi Arabia Ethiopia kuanza tena kuwarejesha makwao raia wake kutoka Saudi Arabia

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Ethiopia inatazamiwa kuanza awamu ya tatu ya kuwarejesha makwao raia wake 70,000 kutoka Saudi Arabia.

Wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia inasema kuwa raia hao "wako katika hali ngumu" katika nchi hiyo ya Ghuba.

Urejeshaji wa utaanza baada ya wiki mbili.

Saudi Arabia ilikuwa imewataka wafanyakazi wa kigeni wanaoishi nchini humo bila haki za kisheria kuondoka au kufungwa jela.

Nchi hiyo inahifadhi takribani Waethiopia 750,000, zaidi ya nusu yao wakiwa nchini kinyume cha sheria, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.

Wanajumuisha wafanyakazi, wanaotafuta kazi na wakimbizi wanaokimbia migogoro katika taifa hilo la Pembe ya Afrika.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamewahi kusema kuwa baadhi ya waajiriwa wa Ethiopia wamekabiliwa na ukiukwaji wa haki zao nchini Saudi Arabia, ikiwemo mateso na mauaji.

Saudi Arabia imewarejesha makwao zaidi ya Waethiopia 350,000 tangu 2017, kulingana na IOM.

Chanzo: Bbc