Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia kujiunga BRICS

Bw Abiy Ethiopia kujiunga BRICS

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi wa ngazi za juu wa serikali ya Ethiopia wamekutana ili kujadili njia za kuweza nchi hiyo kunufaika na uanachama wake ndani ya kundi la BRICS na kuhakikisha inanufaika na manufaa ya pande zote ya kundi hilo.

Taarifa hiyo imetolewa baada ya kikao cha kamati maalumu ya serikali ya Ethiopia ya kufuatilia namna nchi hiyo inavyoweza kunufaika kikamilifu na uanachama wake ndani ya BRICS na faida nyingine zilizomo ndani ya kundi hilo.

Baada ya kuwa mwanachama kimili ya kundi la BRICS, Ethiopia imeunda kamati maalumu ya mawaziri na watu wenye ushawishi mkubwa kitaifa kwa nia ya kuhakikisha uanachama wa nchi katika kundi hilo unakuwa na manufaa yanayotakiwa.

Meles Alem, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia amesema kuwa, nchi yake inashukuru kwa kupata fursa ya kushiriki kwa mara ya kwanza kama mwanachama kamili ya Mkutano wa BRICS uliofanyika hivi karibuni mjini Moscow, Russia.

Mkutano wa BRICS wa Afrika Kusini ulikaribisha wanachama kadhaa wapya

Alem amezungumza na vyombo vya habari na kutoa maelezo kuhusu kushiriki Ethiopia katika mkutano wa Moscow na kusema kuwa huo ni ushindi mkubwa zaidi wa kidiplomasia wa nchi yake.

BRICS ni kifupi cha herufi za awali za majina ya nchi waasisi wa kundi hilo kwa utararibu. Nchi hizo ni Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini yaani (South Afrika).

Wakati wa Mkutano wa 15 wa BRICS uliofanyika Johannesburg, Afrika Kusini, mwezi Agosti 2023, nchi mbalimbali zilikaribishwa kujiunga na kundi hilo. Nchi hizo zilikuwa ni Iran, Misri, Ethiopia, Saudi Arabia na Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati). Nchi hizo zilikuwa wanachama rasmi na kamili wa BRICS terehe Mosi Januari, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live