Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia inakanusha shutuma za Marekani za uhalifu wa kivita

Ethiopia Inakanusha Shutuma Za Marekani Za Uhalifu Wa Kivita Ethiopia inakanusha shutuma za Marekani za uhalifu wa kivita

Tue, 21 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Serikali ya Ethiopia imepinga taarifa ya Marekani inayodai kuwa wanajeshi wake, pamoja na vikosi vya Eritrea na Amhara, walifanya uhalifu wa kivita wakati wa vita vya Tigray vya miaka miwili.

Wizara ya Mambo ya Nje iliitaja kauli hiyo ya Marekani kuwa "ya upande mmoja" na ya "uchochezi" ikisema "mtazamo wa upendeleo na mgawanyiko kutoka Marekani haushauriwi".

Ilisema kwamba "haijafika kwa wakati", inakuja muda mfupi baada ya Ethiopia kuzindua mashauriano ya kitaifa kuhusu sera ya haki ya mpito inayolenga kuleta amani na upatanisho.

"Bila sababu za msingi, kauli hiyo inaonekana kumuondolea mtu hatia kutokana na tuhuma fulani za ukiukwaji wa haki za binadamu kama vile ubakaji na aina nyingine za ukatili wa kijinsia licha ya kuwepo kwa ushahidi wa wazi na mwingi kuhusu hatia yake," ilisema wizara hiyo.

Ilisema taarifa hiyo ya Marekani "itatumika kuendeleza kampeni zenye mgawanyiko mkubwa kati ya jamii moja na nyingine nchini humo".

Siku ya Jumatatu, Marekani ilisema imeamua kwamba pande zote zinazopigana katika vita vya kikatili kaskazini mwa Ethiopia zilifanya uhalifu wa kivita.

Pia ilishutumu vikosi vya Ulinzi vya Ethiopia na Eritrea pamoja na vikosi vya Amhara kwa kufanya uhalifu dhidi ya binadamu ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji na aina nyingine za unyanyasaji wa kingono na mateso.

Chanzo: Bbc